

Originally published by Taifa Leo — Read the original article →

PROFESA David Ndetei amepinga kuachiliwa kwa aliyekuwa mkewe Rose Mbithe Mulwa na watoto wao wawili, Chris na Angela, wanaoshtakiwa kwa mauaji ya mkewe, Dkt Victoria Mutiso.
Akitoa ushahidi katika Mahakama Kuu ya Milimani mbele ya Jaji Alexander Muteti, profesa huyo alisema anahofia maisha yake na ya familia yake ikiwa washukiwa hao wataachiliwa kwa dhamana.