

Originally published by Taifa Leo — Read the original article →

Polisi wamewahakikishia wakazi wa Likoni, Mombasa, kuwa eneo hilo liko salama na hakuna amri ya kutotoka nje usiku iliyotolewa kufuatia tukio la usalama lililosababisha kifo cha afisa wa kaunti na polisi mmoja kujeruhiwa.
Katika taarifa aliyotoa Oktoba 30, 2026, Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Pwani Ali Nuno alisema tukio hilo lilitokea Jumatatu, Oktoba 26, maafisa walipokuwa wakitekeleza majukumu yao.