

Originally published by Taifa Leo — Read the original article →

Jumapili inapowadia, makanisa mengi hujaa waumini, lakini katika viti hivyo kuna pengo linalozidi kuonekana: wanaume. Ingawa baadhi yao huendelea kuhudhuria ibada, wengine wamepunguza safari za kanisani, huku wengine wakiamua kabisa kubaki nyumbani na kuacha familia zao ziende kuabudu.
Sababu zinazowafanya wanaume kujitenga na kanisa ni nyingi. Kwa baadhi yao, ni shughuli za kutafuta riziki na majukumu ya familia. Wengine wamekatishwa tamaa na jinsi wanavyotendewa kanisani, tofauti za kitamaduni au lugha, huku wengine wakihisi hawapewi nafasi ya kushiriki kikamilifu katika maisha ya waumini.