

Originally published by Taifa Leo — Read the original article →
Election process

WAZIRI wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen alikabiliwa na maswali mazito kutoka kwa wabunge kuhusu ongezeko la visa vya utekaji nyara na uhuni kabla ya uchaguzi mkuu ujao.
Alipofika mbele ya bunge kujibu maswali, wabunge walimshutumu Waziri kwa kutojitahidi vya kutosha kudhibiti utamaduni wa uhuni unaoshamiri katika mikutano mingi ya kisiasa na kukosa kujibu kuhusu watu walioripotiwa kutoweka.