

Originally published by Taifa Leo — Read the original article →

WANAFUNZI katika vyuo vikuu vya umma wanaendelea kuathirika kufuatia mgomo wa wahadhiri unaoingia wiki ya tatu, huku wahadhiri wakisisitiza hawatasitisha mgomo hadi matakwa yao yatimizwe.
Wanafunzi wamelalamikia gharama ya maisha bila masomo, huku wakitaka serikali na vyama vya wafanyakazi kutatua mzozo huo.